Tutumie message yenye neno"KAMPUNI" Whatsapp namba +255764530882 kupata maelezo zaidi juu ya huduma yetu* Karibu Sana TJ CONSULT & CO.LTD kwa kazi zote za Graphics design ... Tuna design Logo, Company profile
Habari Mjasiliamali na mpambanaji, Inawezekana bado
unajiuliza na kujishauri kuhusu umiliki wa kampuni au urasimishaji wa biashara
zako lakini bado hujafikia muafaka, na pengine hujawahi hata kufikiria kabisa
na hapa huenda ikawa ni mara yako ya kwanza kufahamu kuhusu makampuni, hali
hiyo hupelekewa na sababu mbalimbali ikiwemo kutokujua kabisa, yaani mtu
mwingine akisikia neno ‘Kampuni’ tayari yanamuijia kichwani kwake majengo
makubwa, magari, wafanyakazi wengi watanashati, akaunti ya fedha benki yenye pesa
nyingi, n.k. hivyo mtu huyo hujiona yeye sio hata wa kulitaja neno kampuni.
Pia sababu nyingine kutokuelewa ni namna gani biashara zake
zinaweza kusajiliwa na kuendeshwa kama kampuni, na zaidi ni kutokuelewa umuhimu
wa kuwa na kampuni, yaani unakuta mtu anafanya biashara nyingi na kubwa mfano
kusafirisha mbao kutoka mkoa wa Iringa kuleta Jijini Dar es Salaam, au kutoa
samaki Mwanza kuleta Dar es Salaam, au biashara ya kukopesha pesa, n.k. lakini
anaona biashara zinakwenda vizuri tu na hivyo asione hata umuhimu wa
kuzirasimisha biashara zake.
Unapoamua kufanya biashara ni vema kuzingatia mfumo wa usajili
wa biashara yako na kuamua vema ili kufanya biashara katika mazingira mazuri
hususani ya kisheria, ndiyo sababu TJ CONSULT & CO.LTD huwa tunawashauri
kwa weledi wale wanaosajili biashara zao ili wafanye maamuzi sahihi. Kwa
kifupi, unaweza kusajili Jina la biashara, mfano ‘Ifakara intersperses’, endapo
nikiwa nafanya biashara ya kusafirisha mizigo, au ‘Ifakara Microcredit’ endapo
ninafanya biashara ya kukopesha pesa, na nitaruhusiwa kuendesha shughuli za
biashara (Business activities) kuanzia moja mpaka Nne tu, endapo nimesajili
Jina la biashara.biashara
*Lakini leo nitajikita katika Kampuni, na mada ya Kampuni ni
kubwa mno, ila nitakufafanulia faida chache muhimu za kuisajili biashara yako
kama kampuni, kwani wengi huuliza, “kuna faida gani za kuwa na kampuni?”*
kama nilivyotangulia kusema hapo juu kuwa jina la biashara
linakupa ruhusa ya kufanya shughuli za biashara zisizozidi nne, tofauti na
kampuni ambapo unaweza kuorodhesha shughuli za biashara mpaka 50, yaani hata
zile ambazo unatarajia kuzifanya kipindi kijacho, zinaweza kutambulika sasa na
hapo baadae likabaki suala la upatikanaji wa leseni ya biashara hiyo kwenye
halmashauri za manispaa au wizarani pamoja na vibali husika kutoka kwenye
mamlaka za serikali, mfano TFDA, TBS na kadhalika.
Moja kwa moja tuangalie umuhimu wa kusajili kampuni, Mara kwa
mara huwa napokea simu za wateja wetu wengi sana wengine wannitumia ujumbe,
wengine hunicheki whatsapp, wengine kwenye E-mail yangu, maswali wanayoniuliza
ni kuhusu faida za kufungua kampuni, huwa nawaeleza kwa ufupi lakini huwa
wanaonekana kutaka kufahamu zaidi suala zima la kodi, kwasababu suala hili la
kodi limekuwa likiulizwa na wengi sana, pia wafanya biashara
wengi wamekuwa wakihitaji kufahamu kuhusu kodi za makampuni, wajasiriamali
na wafanya biashara na wengine wengi nimekuwa na majadiliano nao kuhusu
suala hili, nitajitahidi kueleza kwa undani na kwa ufupi kama ifuatavyo:
Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa
kodi (faida) ya asasi kama vile makampuni yenye dhima ya ukomo. Kampuni yenye
dhima ya ukomo (Limited Liability company) inalipa kodi ya shirika (Corporate
Tax) ambayo ni 30% kwa viwango vya sasa kutokana na Sheria ya mapato
iliyofanyiwa mapitio mwaka 2008 na kodi hii hukokotolewa kwenye faida ya mwaka,
hivyo basi, kampuni itakuwa na unafuu mkubwa kwenye kiwango hiki ukilinganisha
na endapo biashara hiyo ingekuwa ina umiliki binafsi(Jina la biashara), hasa
hasa pale ambapo kampuni inazidi kukua na kuongeza shughuli za biashara.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), mapato
yanayotozwa kodi (faida) katika kodi ya makampuni yanahusisha:
1. Faida inayotokana na shughuli za biashara,
2. Faida inayotokana na uwekezaji (isipokuwa migawanyo ya faida
ambayo imetozwa kodi tofauti kama kodi ya mwisho),
3. Kodi inayotokana na mapato ya makampuni yenye hasara za muda
mrefu ambazo hazijasamehewa kwa miaka mitatu mfululizo.
Mpenzi msomaji wa makala hii, fahamu kwamba zipo faida nyingi
zitokanazo na uendeshaji biashara kama kampuni, kwani makampuni hunufaika na
misamaha ya kodi pamoja na mapunguzo ya kodi kutokana na aina ya shughuli
mbalimbali ambazo inajihusisha nazo.
Kwa mfano, kwa mujibu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),
Kampuni mpya iliyoanzishwa na ambayo inajihusisha na utengenezaji wa madawa ya
binadamu na bidhaa za ngozi na ina mkataba wa makubaliano na Serikali ya
Jamhuli ya Muungano wa Tanzania itatozwa kodi kwa kiwango cha 20% kwa kipindi cha
miaka mitano mfulizo kutoka mwaka walipoanza uzalishaji, hii ni pungufu ya 10%,
pia kama kampuni haijapata faida, itaandaa vitabu vyake vya mahesabu na
kuviwasilisha kwenye mamlaka ya mapato na haitalipa chochote, kodi itatozwa
kwenye faida kama ilivyoainishwa kwenye sheria na si vinginevyo, tofauti na
biashara binafsi(sole proprietors).
Watu binafsi (sole proprietors) hukadiriwa kodi kutokana na
mauzo yao, kwa mfano;
Kwa mtanzania (bara) kodi kwa mtu binafsi endapo mapato yake
yanazidi Shs 720,000/= kiwango cha kodi anayotozwa ni Shs 98,100/= jumlisha na
30% ya mapato yanayozidi Shs 720,000/=, lakini kwa kampuni, huenda mapato
yakawa ni hiyo hiyo Shs 720,000/= kwa mwezi, na gharama na matumizi vikawa ni
Shs 300,000/=, kwa hiyo faida ni Shs 420,000/=, kwa hiyo kwa mwezi huo kwa
kampuni kodi itakokotolewa kwa kupata 30% ya faida, yaani Shs 420,000/= ambayo
ni Shs 126,000/=, tofauti na mtu binafsi ambaye atalipa Shs 98,100/= jumlisha
30% ya mapato yanayozidi 720,000/=, tuseme ni Shs 800,000/= ambayo ni Shs 240,000/=,
hivyo kutakiwa kulipa kiasi cha Shs 338,100/=. japo kwa mwaka mapato yasiyozidi
Shs 2,040,000/= kwa watu binafsi hayatozwi kodi, lakini kwa hali ya kawaida ya
biashara na bei ya vitu na huduma kuwa juu, ni rahisi kwa mapato kuzidi kiwango
hicho pamoja na kupata faida kidogo, lakini kwa kuwa ni mtu binafsi mzigo wa
kodi ukakuelemea vile vile.
Kwa hiyo, hapa tunaona unafuu wa kusajili kampuni, na ndivyo
ambavyo Shinebright Consulting tunawashauri wawekezaji, na ukihitaji kufahamu
zaidi wasiliana nasi au tutembelee ofisini.
Pia, Unapoisajili biashara yako kuwa kampuni unapunguza hatari
ya kuwepo kwa mvutano wa kimaslahi baina ya waanzilishi, kwani wamiliki wa
kampuni maslahi yao kwenye kampuni husika ambayo wanaimiliki yanakoma kulingana
na idadi ya hisa wanazozimiliki, au kiwango cha uwekezaji kutokana na hisa
walizozinunua, na si vinginevyo. Tumezoea kuwepo na makubaliano holela ya mdomo
au maandishi kwamba mtu A na mtu B wamekubaliana watafanya biashara fulani
kisha watagawana faida, halafu baadae wanaanza kuingia kwenye migogoro kwamba
huyu anasema biashara ni ya kwake na yule anasema ni ya kwake, au katika
kugawana faida kila mmoja anaweza kumzidi mwenzake na hupelekea watu kugombana
hata kusababisha hasara kubwa, lakini kama watu wameamua kufanya biashara kwa
kuisajili kwanza kuwa kampuni, biashara hiyo inakuwa na utaratibu rasmi wa
kisheria katika kuisimamia na anapotaka kujiondoa mmoja wapo, unafuatwa
utaratibu rasmi ambao upo kwa mujibu wa sheria, na si vinginevyo.
Hivyo basi, kusajili kampuni kunaondoa migogoro mingi ambayo
inaweza kujitokeza baadae, hasa biashara inapokua kubwa sana au inapoonekana
kukwama kukua.
Hali kadhalika kusajili kampuni kunapelekea kuwepo na mazingira
rafiki ya kukuza mtaji. Kuongeza mtaji wa kampuni kunaweza kusaidia katika
upanuzi wa biashara au kupelekea ukuaji. Taratibu za kitaalamu na kisheria
zimeainisha namna nzuri za kuongeza mtaji aidha kwa kuuza hisa zilizobakia
kwenye kampuni kwa wamiliki waliopo ili kuongeza mtaji, au kwa kuongeza
wanahisa wapya na kununua hisa za kampuni ili kuongeza mtaji, na pia ni rahisi
hata kuwakaribisha wawekezaji wengine ndani au nje ya nchi wakanunua hisa na
kuongeza mtaji bila kuathiri shughuli za kampuni.
Sio rahisi kama mtu unafanya biashara ambayo haijasajiliwa kuwa
kampuni, kuwakaribisha watu wengine kuwekeza pesa zao kwako, usalama wa
kuwekeza pesa ni pale ambapo biashara imesajiliwa kama kampuni, kwani hata
katika macho ya kisheria kampuni inatazamwa kama taasisi nyingine tofauti na
wamiliki wa kampuni hiyo (separate entity).
Jambo lingine muhimu kabisa ni kuwepo kwa ukomo wa dhima binafsi
(Limited liability).
Kampuni mbele ya macho ya sheria ni taasisi inayosimama yenyewe
tofauti na wamiliki wa kampuni hiyo (separate legal entity), na kampuni inaweza
kushitaki au kushitakiwa mahakamani (veil of incorporation), hivyo basi, endapo
biashara inapata misukosuko katika uendeshaji, umiliki au uwekezaji, n.k.
inaweza kuwajibika yenyewe na wamiliki wa kampuni hiyo wasipoteze kitu chochote
isipokuwa tu uwekezaji wao kwenye kampuni hiyo. Mfano; katika biashara, mmekopa
pesa benki au kwenye taasisi yoyote ya fedha na biashara ikashindwa kufikia
malengo ikajikuta inaingia kwenye madeni makubwa, ni kampuni ndiyo
itakayowajibika kwenye madeni hayo, na wamiliki wa kampuni watakachopoteza ni
uwekezaji wao kwenye kampuni husika. Pia endapo bidhaa au huduma zilizotolewa
zimeisababishia hasara kampuni, itakayowajibika ni kampuni yenyewe. Hii ni
tofauti na biashara binafsi (Sole proprietorship) ambapo mmiliki wa biashara
anawajibika moja kwa moja yeye mwenyewe kwasababu kisheria ni yeye mwenyewe
ndiye anayetambuliwa na si vinginevyo.
Mwisho tuangazie suala muhimu sana nalo ni kujitambulisha na
kujitengenezea hadhi kibiashara, jambo ambalo linaweza kuboresha mahusiano mazuri
baina ya kampuni yako na wateja (Branding). Leo tunaona makampuni makubwa kama
Vodacom, IPP Media, Mbeya Cement, CRDB n.k. namna yalivyojitengenezea namna ya
kutambulika kwa wateja wao, unapolisikia tu jina la kampuni mojawapo limetajwa
unapata picha halisi na kubwa juu ya biashara ya kampuni hiyo kwa uharaka.
Kuendesha biashara iliyosajiliwa kama kampuni pia kunakupelekea kuaminika na ni
rahisi hata kuingia mikataba mikubwa aidha na makampuni mengine au na serikali.
Kwa mfano, serikali inatangaza zabuni ya ujenzi wa barabara na mradi huo
gharama yake ni Shs 30,000,000/=, pesa hizo zote sio rahisi kuingia mkataba na
mtu binafsi au watu wachache binafsi wasio rasmi kisheria, lakini ni rahisi
kuingia mkataba na kampuni, na pia hata kukopeshwa kwenye mabenki na makampuni
ya fedha mikopo mikubwa ya biashara ni rahisi endapo mmesajiliwa kama kampuni
kuliko binafsi (individuals).
Leo TJ CONSULT & CO.LTD imekuwa na nafasi kubwa ya
kuhudhuria mikutano mikubwa na kukutana na wawekezaji wa nje wengi na wa ndani wengi
ambao wanamtazamo mpana kibiashara na tumekuwa tukiwashauri wawekezaji wa ndani
na nje ya nchi namna ambavyo wanaweza kunufaika endapo watasajili biashara zao
kuwa kampuni na sio kuziendesha kiholela au kienyeji.
Jambo moja ambalo nilitaka kulisahau, unaposajili kampuni
inakurahisishia wewe hata namna ya kuirithisha biashara, kwa mfano; Baba na
mama mmesajili kampuni na mtoto wenu amefikisha umri wa miaka 18, mnaweza
kumuongeza kama mwenye hisa (Shareholder) na biashara zikaendelea kama kawaida,
wakati anaendelea kupata elimu, anakuwa anafahamu fika kwamba anasoma ili
asimamie biashara ambayo yeye mwenyewe ni mmiliki halali wa sehemu ya biashara
hiyo kutokana na kiwango cha hisa anazozimiliki, hivyo kumfanya asome kwa bidii
bila kuwa na hofu juu ya soko gumu la ajira.
Zipo faida nyingi na muhimu sana za kusajili biashara yako kuwa
kampuni, usichelewe kwani wakati ni sasa, rafiki yangu mmoja nilimsikia akisema
kuwa “Kusajili kampuni ni lazima uwe na gari kwanza, lazima” aliongea kwa
kusisitiza, lakini kwa kumsaidia na kwa faida ya wengi, kusajili kampuni zipo
taratibu maalum zilizowekwa na mamlaka husika yaani BRELA (Wakala wa usajili wa
makampuni na majina ya biashara), na sisi kama washauri nafasi yetu ni
kukushauri uwe na ufahamu juu ya makampuni na uendeshaji wake, umuhimu wa
kusajili biashara na kukupa msaada wa kitaalam ili uweze kufanya maamuzi sahihi
na yenye tija, ili kutimiza malengo yako kwa wakati na bila gharama
zinazoepukika.
Mimi ni Business doctor, Life coach na mchambuzi wa masuala ya
biashara na mjasiriamali.
*TJ CONSULT & CO.LTD*
*Kama una wazo la kufanya biashara
hapa Tanzania na ungependa kumiliki kampuni yako au jina la biashara lako,*
huduma yetu ni kukusaidia kufanikisha usajiri wa biashara yako.
Tutumie message yenye neno "KAMPUNI" Whatsapp namnba +255764530882
kupata maelezo zaidi juu ya huduma yetu*
Karibu Sana TJ CONSULT & CO.LTD
kwa kazi zote za Graphics design ... Tuna design Logo, Company profile, kwa
wajasiliamali, Matangazo ya mtandaoni, Business card, rollup banner,catalog,
hotel & restaurant menu, business proposal, company profile na vingine
vingi, Huduma zetu sisi TUNAKUFIKISHIA POPOTE ULIPO.
Call 255626 402 722 OR +255764530882,
WhatsApp no: +255764530882,
TJ Tuna aminika kufanya Graphics
Design kwa Kwa bei zakawaida kabisa kwa asilimia 100% karibuni sana TJ CONSULT
& CO.LTD
*SASA NAHITAJI KUTENGENEZA COMPANY
PROFILE NA KUSAJIRI KAMPANI YANGU,NITAWAPATA WAPI TJ CONSULT & CO.LTD*??
*Tumia hayo mawasiliano hapo chini
kuwasiliana na TJ CONSULT & CO.LTD au fika offisini kwetu Tunapatikana, SONGEA
MFARANYAKI & DODOMA NKUHUNGU;*
Whatsapp & call
+255764530882,+255626 402 722
E-mail:bizewiseconsultancy@gmail.com
*Thanks*
Comments
Post a Comment