Posts

Showing posts with the label Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar

Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar yakimuhusisha mtu asiye maarufu sana, John Okello

Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi na wanamapinduzi wa kweli wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania. Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini ...