Habari Mjasiliamali na mpambanaji, Inawezekana bado unajiuliza na kujishauri kuhusu umiliki wa kampuni au urasimishaji wa biashara zako lakini bado hujafikia muafaka, na pengine hujawahi hata kufikiria kabisa na hapa huenda ikawa ni mara yako ya kwanza kufahamu kuhusu makampuni, hali hiyo hupelekewa na sababu mbalimbali ikiwemo kutokujua kabisa, yaani mtu mwingine akisikia neno ‘Kampuni’ tayari yanamuijia kichwani kwake majengo makubwa, magari, wafanyakazi wengi watanashati, akaunti ya fedha benki yenye pesa nyingi, n.k. hivyo mtu huyo hujiona yeye sio hata wa kulitaja neno kampuni. Pia sababu nyingine kutokuelewa ni namna gani biashara zake zinaweza kusajiliwa na kuendeshwa kama kampuni, na zaidi ni kutokuelewa umuhimu wa kuwa na kampuni, yaani unakuta mtu anafanya biashara nyingi na kubwa mfano kusafirisha mbao kutoka mkoa wa Iringa kuleta Jijini Dar es Salaam, au kutoa samaki Mwanza kuleta Dar es Salaam, au biashara ya kukopesha pesa, n.k. lakini anaona biashara zinakwend...