Kazakh: Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena, baada ya kufukuliwa miaka 50 iliyopita
Kazakhstan itazika tena mabaki ya mwili wa shujaa wa kipekee katika hifadhi ya kihistoria kwa ajili ya watu wa baadae. Matumaini yao ni kwamba vizazi vya baadae watafanikiwa kugundua asili ya mtu huyo. Wanahistoria waligundua mabaki hayo yakiwa yamembatana na silaha za dhahabu safi pamoja na sanaa mbali mbali za thamani wakati wakichimba katika makaburi ya Issyk kusini mwa nchi hiyo mwaka 1969, na hapo hapo wakampa jina la "binadamu wa dhahabu". Tangu uhuru mwaka 1991 amekuwa ni ishara ya urithi wa asili wa taifa huko Kazakhstan. Silaha yake ya dhahabu imekuwa ni kitu cha kujivunia na imehifadhiwa katika hifadhi ya taifa ya Astana, pia hudhuru sehemu mbali mbali duniani kama alama ya tamaduni ya Kazakh. Serikali yazima jaribio la mapinduzi Gabon Kinywaji kinachodaiwa kuwa na 'Viagra' kuchunguzwa Uganda Haki miliki ya picha ...