Jinsi ya Kuandika Ripoti

Uandishi wa ripoti unategemea sana mambo kadha wa kadha kama ilivyoorodheshwa hapa chini:
Ripoti hiyo ni ya aina gani?
  1. Ya Kesi?
  2. Ya Utendaji kazi wa kawaida?
  3. Ya Utafiti?
  4. Ya kuanzisha mradi?
  5. Kusuluhisha migogoro!
  6. Ya shule/chuo
  7. Ya cheo kipi? Afisa, meneja, mkurugenzi
  8. Kwenda kwa nani, afisa, mkurugenzi, bodi
Maswali yanaendelea na majibu yake ndio msingi muhimu wa uandishi wa ripoti
Pamoja na hayo yote, mfumo wa ripoti karibu unafana kwa maeneo muhimu hapa chini:
Mfano ripoti ya Mei 2018
  1. Kasha la nje – Kichwa cha ripoti na mwandishi
  2. Utangulizi
  3. Malengo (Lengo kuu na malengo Mahsusi)
  4. Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa Mei 2018
  5. Kazi zilizotekelezwa kiwango cha utekelezaji na majadiliano yake (Hapa elezea kwa takwimu na au viashiria, takwimu kama unaripooti matokeo yanayohesabika au viashiria kama unaripoti matokeo yasiyohesabika)
  6. Kiambatanisho cha ripoti ya fedha(Hiki kipengele ni muhimu kama unasimamia fedha au utendaji wako ulihusisha matumizi ya fedha)
  7. Kazi zilizofanywa ambazo hazikuwepo kwenye mpango (elezea kama hapo juu)
  8. Habari njema
  9. Changamoto na njia za kutatua
  10. Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa June 2018
  11. Hitimisho – maoni na ushauri wa mwandishi/waandishi
  12. Orodha ya waliopokea nakala ya ripoti (Ofisi, Jina, Cheo)

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)