DIRISHA LA MAOMBI YA MKOPO KWA NJIA YA MTANDAO KUFUNGULIWA JULAI 1, 2019
Tunapenda kuwafahamisha waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao litafunguliwa rasmi Jumatatu, Julai 1, 2019 na kufungwa Alhamisi, Agosti 15, 2019. Maombi yote yatafanywa kupitia mtandao utakaopatikana kupitia www.heslb.go.tz. Kati ya leo (Jumanne, Juni 25) na Julai 1, 2019 wakati dirisha litakapofunguliwa, wanafunzi wanashauriwa kuhakikisha wanakamilisha nyaraka muhimu zinazotajwa katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa 2019/2020’ unaopatikana katika tovuti ya HESLB ( www.heslb.go.tz ). Nyaraka hizo na maelezo mengine ya ufafanuzi pia yanapatikana katika kitabu kidogo cha ‘Maswali na Majibu 26’ kuhusu uombaji mkopo kinachopatikana katika tovuti hiyohiyo. Kwa ajili ya kumbukumbu, nyaraka muhimu ni pamoja na: Nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwombaji wa mkopo iliyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA); Nakala ya ...