Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu
Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu. Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba aliwai kusema “Ndugu zangu sina budi kuwa kumbusha kuwa siku hizi kuna Wakimbizi wa Mazingira, watu wanaharibu mazingira katika maeneo yao na kuhamia maeneo mengine, jitihada za maendeleo zote hazitakuwa na maana kama hatutatunza Mazingira yetu”. Raisi wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alisema “Umaskini na uharibifu wa Mazingira ni watoto mapacha na mama yao ni Ujinga.” Mwanadamu ndio chanzo cha uharibifu wa Mazingira na uharibifu huo unasababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utupaji wa taka ovyo zikiwemo taka za plastiki. Plastiki utengenezwa kwa kiasi kikubwa na malighafi aina ya organic polymers. Polyethylene na nylon ni mfano mzuri wa organic polymers. Kauli mbiu ya mazingira ya mwaka 2018 duniani kote ilisema "Kupiga vita uchafuzi wa plastiki" (Beat Plastic Pollution) na kilele cha kuadhimisha siku hiyo...