Posts

Showing posts with the label Maombi ya Kazi Kupitia Email

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)

Image
Utangulizi Kuelekea maendeleo ya sayansi na teknolojia (teke linalokujia) na hasa kwenye nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) makampuni na waajiri wengi sasa wanataka maombi ya kazi yafanywe kwa email au barua pepe (sio barua pepo) Maombi ya kaz kupitia email husaidia yafuatayo: kuokoa gharama kama za uchapaji na usafiri kuokoa muda wa barua kutoka kwa muombaji mpaka imfikie mwajiri Kuharakisha pia mawasiliano baada ya maombi kutumwa Kama utaomba kazi kupitia email zingatia yafuatayo: Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Theodory Edmund Ngonyani, email iwe hivi. theodoryngonyani@yahoo.com, theodoryngonyani@outlook.com NK. Angalau majina yako mawili yatokee kwenye email ID. Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama dumelamji@gmail.com au dijose@gmail.com NK Tumia pia email zenye kufuata weledi wa kimataifa. Mfano siwashauri watu ...