Posts

Showing posts from January 31, 2019

kama unataka kampuni basi inabidi uwe na mambo yafuatayo

kama unataka kampuni basi inabidi uwe na mambo yafuatayo 1.Wamiliki wasiopungua wawili pamoja na mgawanyo wa umiliki(shares) 2.Mahali walipo Wamiliki (physical location) 3.Sehemu unayotarajia biashara kuwepo(business location) 4.Utatakiwa kuandaa katiba ya biashara yako( kisheria inaitwa Memorandum and Article of Association) 5.Unaweza andaa mwenyee au ukatafuta Mwanasheria 6.Usajiri unafanywa online kupitia BRELA 7.Jina la kampuni lisilo fanana na kampuni yoyote iliyosajiliwa BRELA 8.Gharama ya usajili italingana na mtaji wako 9.Hatua zingine zinaweza fuata baada ya hii...km kutafuta leseni..TIN number n.k 10.Haya ni mawazo yangu wadau wengine wanakaribishwa kuchangia Kwa msaada zaidi unaweza nipigia kupitia 0764530882 NoTE: Remember any business to succeed is all about branding and Serious planning karibu Kwa msaada zaidi kama utaridhia ukinipa mahitaji yoote yahusuyo usajili wa kampuni ...naweza kukufanyia procedure zote unakabidhiwa kampuni mkononi(full legal docu

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)

Image
Utangulizi Kuelekea maendeleo ya sayansi na teknolojia (teke linalokujia) na hasa kwenye nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) makampuni na waajiri wengi sasa wanataka maombi ya kazi yafanywe kwa email au barua pepe (sio barua pepo) Maombi ya kaz kupitia email husaidia yafuatayo: kuokoa gharama kama za uchapaji na usafiri kuokoa muda wa barua kutoka kwa muombaji mpaka imfikie mwajiri Kuharakisha pia mawasiliano baada ya maombi kutumwa Kama utaomba kazi kupitia email zingatia yafuatayo: Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Theodory Edmund Ngonyani, email iwe hivi. theodoryngonyani@yahoo.com, theodoryngonyani@outlook.com NK. Angalau majina yako mawili yatokee kwenye email ID. Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama dumelamji@gmail.com au dijose@gmail.com NK Tumia pia email zenye kufuata weledi wa kimataifa. Mfano siwashauri watu

Utangulizi Kuhusu MEMART

Image
Utangulizi Kuhusu MEMART   Namna Rahisi ya Kuandika MEMART – Memorandum and Article of Association Zifuatazo ni hatua na mambo muhimu ya kuyazingatia unapotaka kundika Memart MEMART ina sehemu kuu mbili Memorandum of Association Articles of Association Memorandum of Association Hii nis ehemu ya kwanza kabisa ya MEMART ambayo ina sehemu kuu nne: Jina la kampuni Ofisi ya kampuni Madhumuni ya kuanzisha kampuni Majina, anuani, idadi ya hisa na sahihi za wanahisa Sahihi ya mwanasheria na muhuri wake kama shahidi Articles of Association Hii ni sehemu kuu ya pili ya MEMART ambayo kwa ukweli inatafsiri tu sheria ya Makampuni ya Mwaka 2002 na maboresho yake kama ilivyotolewa kwa miaka tofauti. Inashauriwa kumtumia mwanasheria aliyebobea kwenye haya mambo ya kisheria kwa upande wa makampuni ili akusaidie vizuri namna ya kuiweka sehemu hii Pamoja na mambo mengi ya kisheria sehemu hii pia inatoa fursa ya kuorodhesha wakurugenzi wa kwanza wa kampuni, majina, anuani,

Vigezo vya kupata mkopo Benki

Vigezo vya kupata mkopo Benki Uwe na shughuli/biashara rasmi…. hii inammanisha kuwa lazima uwe na leseni ya biashara, leseni hizi hutolewa na afisa biashara wa wilaya yako. Uwe na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN), hii itasaidia kudhibitisha kuwa wewe ni mlipa kodi Uwe na dhamana, yaweza kuwa nyumba, shamba, kiwanja Uwe na barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa Uwe na kitambulisho Uwe na akaunti xxxxx au benki nyingine yoyote. Kama una akaunti benki nyingine utatakiwa kupeleka taarifa ya akaunti yako (Bank statement).

Jinsi ya Kuingiza Taarifa za Kampuni Kwenye Website ya BRELA

UTANGULIZI Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi. Hatua zifuatazo zinawawezesha wamiliki, wasimamizi wa makampuni na biashara kuingiza taarifa zao kwenye tovuti ya BRELA Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za kampuni chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu  Hatua #1: Taarifa za msajili Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la  kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa