TAARIFA KWA UMMA KUFUTWA KWA MAKAMPUNI (LIMITED BY GUARANTEE) YENYE KUFANYA SHUGHULI ZILIZOAINISHWA KWENYE SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGO’S)












 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI
(Ofisi: Jengo la Ushirika Mtaa wa Lumumba)
Simu: +255-22-2181344, 2180113, 2180141
2180048,
Nukushi:+255-22-2180371
Barua Pepe: usajili@brela.co.tz
ceo@brela.go.tz
brela@brela.go.tz
S.L.P. 9393
DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA UMMA
KUFUTWA KWA MAKAMPUNI (LIMITED BY GUARANTEE) YENYE KUFANYA SHUGHULI ZILIZOAINISHWA KWENYE SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGO’S)
1. Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Makampuni (SURA.212 ) yaliyofanyika kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na. 3) ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa tarehe 30 Juni 2019, Jukumu la kusajili Makampuni yanayofanya shughuli kwa lengo la kutogawana faida na ambazo hazina malengo ya kukuza biashara” promotion of commerce” limehamishiwa kutoka kwa MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA) kwenda Kwa Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali
(NGO’s).
2. Kufuatia mabadiliko haya, MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA) anapenda kuufahamisha umma na wamiliki wote wenye Makampuni ambayo yanafanya shughuli kwa lengo la kutogawana faida na ambayo hayana malengo ya kukuza biashara” Promotion of commerce” kwamba kampuni hizo zote zitafutwa kwenye daftari la Msajili wa Makampuni baada ya miezi miwili kuanzia tarehe 30 Juni, 2019 na zitakuwa zimehamishiwa kwa Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali
(NGO’s).
3. Hivyobasi, Kuanzia tarehe ya tangazo hili, MSAJILI WA MAKAMPUNI hatasajili kampuni yoyote ambayo inafanya shughuli kwa lengo la kutogawana faida na ambayo haina malengo ya kukuza biashara” Promotion of Commerce”.
4. Vilevile kuanzia Tarehe 1 Septemba, 2019, MSAJILI WA MAKAMPUNI
hatatunza kumbukumbu za kampuni yoyote iliyosajiliwa kwa lengo la
kutogawana faida na ambayo haina malengo ya kukuza biashara” promotion of
commerce”.
5. Kwa taarifa hii tunawaomba wateja wote wawasiliane na Msajili wa Mashirika
yasiyo ya Kiserikali ( NGO’s) kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kuwasilisha
maombi yao ya usajili kwa Makampuni ambayo yamesajiliwa na Msajili wa
Makampuni (BRELA) na yanatakiwa kuhamia kwa Msajili Mashirika yasiyo ya
Kiserikali ( NGO’s)kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
(Na. 3) ya mwaka 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),
Dar es Salaam
12 Julai, 2019

unaswali lolote usisite kutuandikia kupitia barua pepe yetu hii

etj.prof@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)