AGIZO KUAPDATE TAARIFA ZA KAMPUNI/JINA LA BIASHARA NDANI YA SIKU 90 NJOO TUKU SAIDIE

TAARIFA KWA UMMA
Dar es Salaam, 27 septemba 2019
Hii ni kuutarifu umma kuwa WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA
NA LESENI (BRELA) inaendelea na zoezi la ihuishaji wa Taarifa za
makampuni yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa Kieletroniki. Tunapenda
kutoa taarifa kwa umma na watu wote wenye makampuni na Majani ya
Biashara kuhakikisha wanauhisha taarifa za makampuni yao na Majina
ya Biashara katika kipindi cha SIKU 90 kuanzia tarehe ya tangazo hili.
MAHITAJI NA TARATIBU ZA UHUISHAJI WA TAARIFA
• Muombaji awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN) ambayo
husaidia kufungua akaunti ya BRELA kwenye tovuti ya Wakala.
• Endapo maombi ni ya Kampuni unatakiwa kuwa na Namba ya
Utambulisho wa Mlipa Kodi (Tax Identification Number –TIN) ya
kila Mkurugunzi na ya Kampuni husika.
• Kupitia taarifa za Kampuni na kuhakikisha zipo sahihi kisheria na
kikanuni.
• Kujaza ‘Consolidated form’ katika mfumo wa ORS na kupakia taarifa
zozote zinazohitajika mfano Taarifa ya Mwaka (Annual returns),
mabadiliko yaliyotokea katika kampuni ambayo hayakuletwa hapo
awali.
• Kuweka saini katika fomu zote, kuweka saini kwenye ‘Consolidated
form’, Kuzipakia katika akaunti na kutuzima BRELA kwa njia ya
mtandao.
• Baada ya Kukamilisha kuhuisha (Updated) taarifa itahakikiwa na
kupatiwa Ankara ya Malipo na muombaji atatakiwa kulipia Benki
au kwa njia ya simu.
KATIKA ZOENZI HILI BRELA INASISITIZA MAMBO YAFUATAYO:
Wakati zoezi hili linaendelea BRELA inapenda kutoa kwa kifupi taratibu
za namna ya kutumia huduma za BRELA kwa njia ya mtandao.
• Kuwasilisha taarifa sahihi zinazoendana na taarifa zilizopo katika
masijala ya usajili.
• Kufanya zoezi wenyewe au kuwatumia wenye weledi na uelewa wa
kutosha wa sheria za sajili mbalimbali.
• Kuwasilisha taarifa zilizokamilika
• Kuzingatia maelekezo ya Marekebisho kwenye maombi
yanayorudishwa kwao.
• Kuambatisha nyaraka sahihi kwa Kampuni zenye mabadiliko mbali
mbali.
• Kutorudia kosa lile lile au kuongeza makosa mengine baada ya
kupewa maelekezo ya masahihisho.
• Kutoa taarifa za kweli na uhakika na kuzingatia marekebisho
wanayopewa ili kuleta ufanisi na uharaka.
• Kuhakikisha kuwa anayefungua akaunti kwenye mfumo wa ORS
wa BRELA ni Mmiliki wa hisa katika Kampuni au Mwenye jina la
Biashara na pia unashauriwa kutunza Jina na neno la siri (User
name na Password)
TUPIGIE AU UJUMBE(WHATSAPP) 0764 530 882 au etj.prof@gmail.com    24hrs

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)