Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi/Maombi ya Kazi Je ulishawahi kuandika barua ya maombi ya kazi na kutuma kwa waajiri wengi na wote au wengi ya hao hawakukujibu hata kama unajua unazo sifa za hiyo kazi? Jibu la hapo ni rahisi Uandishi wa barua zako una shida Barua ya maombi ya kazi iwe na sura hii Wewe nani Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi) Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani) Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wako
Uandishi wa ripoti unategemea sana mambo kadha wa kadha kama ilivyoorodheshwa hapa chini: Ripoti hiyo ni ya aina gani? Ya Kesi? Ya Utendaji kazi wa kawaida? Ya Utafiti? Ya kuanzisha mradi? Kusuluhisha migogoro! Ya shule/chuo Ya cheo kipi? Afisa, meneja, mkurugenzi Kwenda kwa nani, afisa, mkurugenzi, bodi Maswali yanaendelea na majibu yake ndio msingi muhimu wa uandishi wa ripoti Pamoja na hayo yote, mfumo wa ripoti karibu unafana kwa maeneo muhimu hapa chini: Mfano ripoti ya Mei 2018 Kasha la nje – Kichwa cha ripoti na mwandishi Utangulizi Malengo (Lengo kuu na malengo Mahsusi) Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa Mei 2018 Kazi zilizotekelezwa kiwango cha utekelezaji na majadiliano yake (Hapa elezea kwa takwimu na au viashiria, takwimu kama unaripooti matokeo yanayohesabika au viashiria kama unaripoti matokeo yasiyohesabika) Kiambatanisho cha ripoti ya fedha(Hiki kipengele ni muhimu kama unasimamia fedha au utendaji wako ulihusisha matumizi ya fedha) Kazi zilizofanyw...
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI WA ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI 1, tumia Lugha inayojulikana na mataifa Mengi. Hapa tunashauriwa kutumia Lugha ya kingereza, Kwan ndiyo inayotambuliwa na wafadhili wengi. May be Ukiwa unaandikia kwa wafadhili wa ndani ya nchi. 2. Fuata hatua Za maombi - Hii ni kwasababu wafadhili wengi hupenda kutumia muundo wao ambao utaujaza kwa kujibu maswali yaliyoainishwa katika muundo huo ulioandaliwa. ( Tutajifunza kwenye practical ) - Lakini ikiwa Hakuna muundo ulioandaliwa na agencies basi utaandika kwa kufuata vipengere muhimu vya kuvifuata katka uandishi uo ( tutaviangalia soon ). 3. Kuwa makini na tarehe ya Mwisho katika kutuma maombi ya proposal - kosa kubwa linalofanywa na watu wengi ni kutuma maombi tarehe na dakka Za Mwisho. Hii inapelekea mfadhili kutoisoma/ kuifuatilia proposal yako vizuri. 4. Kujua kanuni na taratibu Za mfadhili katika utoaji wa ruzuku- kuzifahamu taratibu na kanuni ni hatua ya msingi katika kupata r...
Comments
Post a Comment