Barua ya Kuomba Kazi
    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi/Maombi ya Kazi    Je  ulishawahi kuandika barua ya maombi ya kazi na kutuma kwa waajiri wengi  na wote au wengi ya hao hawakukujibu hata kama unajua unazo sifa za  hiyo kazi?  Jibu la hapo ni rahisi  Uandishi wa barua zako una shida  Barua ya maombi ya kazi iwe na sura hii   Wewe nani  Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi  Unafikiri  wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi  hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti  vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi  kwani na wao wanazo tena kukuzidi)  Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi  Acha  mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe  (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba,  mama, baba na marafiki au jirani)  Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wako   
Comments
Post a Comment