Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi/Maombi ya Kazi Je ulishawahi kuandika barua ya maombi ya kazi na kutuma kwa waajiri wengi na wote au wengi ya hao hawakukujibu hata kama unajua unazo sifa za hiyo kazi? Jibu la hapo ni rahisi Uandishi wa barua zako una shida Barua ya maombi ya kazi iwe na sura hii Wewe nani Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi) Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani) Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wako
MKATABA WA PANGO LA CHUMBA CHA BIASHARA: Mimi ………….. wa S.L.P. …………. – (eneo) mkazi wa ………………. leo tarehe …………. 2019 nimeingia mkataba wna Ndugu ………………… wa S.L.P. ………….. – Songea kupanga chumba cha biashara kwenye nyumba iliyopo …………….. Shughuli ya biashara itaanza tarehe …………….. baada ya kukamilisha taratibu za kuanza biashara, hivyo pango litahesabika kuanzia tarehe hiyo. Mkataba huu ni wa miezi mitatu baada ya hapo nitaamua kuendelea au vinginevyo. Pango la chumba kwa mwezi ni Tshs: ……………./= kwa mwezi. Huduma za umeme. na maji zitategemea matutumizi kupitia metre separator au mita yangu mwenyewe. Mkataba huu nimeingia nikiwa na akili timamu na kushuhudiwa na: - ……………………………. ………………………………… …………………………….. (……………….) ...
Uandishi wa ripoti unategemea sana mambo kadha wa kadha kama ilivyoorodheshwa hapa chini: Ripoti hiyo ni ya aina gani? Ya Kesi? Ya Utendaji kazi wa kawaida? Ya Utafiti? Ya kuanzisha mradi? Kusuluhisha migogoro! Ya shule/chuo Ya cheo kipi? Afisa, meneja, mkurugenzi Kwenda kwa nani, afisa, mkurugenzi, bodi Maswali yanaendelea na majibu yake ndio msingi muhimu wa uandishi wa ripoti Pamoja na hayo yote, mfumo wa ripoti karibu unafana kwa maeneo muhimu hapa chini: Mfano ripoti ya Mei 2018 Kasha la nje – Kichwa cha ripoti na mwandishi Utangulizi Malengo (Lengo kuu na malengo Mahsusi) Kazi zilizopangwa kwa mwezi wa Mei 2018 Kazi zilizotekelezwa kiwango cha utekelezaji na majadiliano yake (Hapa elezea kwa takwimu na au viashiria, takwimu kama unaripooti matokeo yanayohesabika au viashiria kama unaripoti matokeo yasiyohesabika) Kiambatanisho cha ripoti ya fedha(Hiki kipengele ni muhimu kama unasimamia fedha au utendaji wako ulihusisha matumizi ya fedha) Kazi zilizofanyw...
Comments
Post a Comment