Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yatangaza nafasi 4 za kazi

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke anawatangazia Wananchi/Watanzania wote wenye sifa zinazotakiwa kuomba kujaza nafasi mbalimbali za kazi kama zilivyoainishwa hapo chini:-

AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (Nafasi 1)

SIFA/ELIMU/UJUZI


  • Elimu ya kidato cha Nnne (IV) , au Kidato cha Sita (VI,)
  • Cheti(Astashahada) cha, Utawala, Sheria, Elimu yajamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi kutoka Chuo cha Serikali ya Mitaa Hombolo,Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Ataanza mshahara TGS B kwa mujibu wa viwango vya Serikalini.

UMRI
Waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.

MAELEZO YA JUMLA
Maombi yote yawasilishwe yakiwa yameambatanishiwa na CV pamoja na nakala za vyeti vya kuhitimu elimu na mafunzo (vyeti vinavyoonyesha kiwango cha kufaulu na sio 'leaving certificate')

MUHIMU
Muombaji anatakiwa atume vyeti vyake halisi na halali kwani uhakiki utafanyika katika vyuo alivyopitia pamoja na Baraza la Mitihani. Udanganyifu wowote ukibainika hatua za kisheriaz zitachukuliwa

KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (Nafasi 1)

SIFA/ELIMU/UJUZI

  • Elimu ya kidato cha IV.
  • Waliohudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya III.
  • Waliofaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika 1.
  • Waliopata mafunzo ya Kompyuta kutoka katika Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programme ya windows/Microsoft Office/Internet/Email na Publisher.
KAZI NA MAJUKUMU
  • Kuchapa barua/taarifa na nyaraka za kawaida.
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanaweza kushunghulikiwa.
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake, na ratiba za kazi zingine zilizotangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumwarifu mkuu wake kwa wakati unapohitajika.
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shunghuli za kazi hapo Ofisini.
  • Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumwarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
  • Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu inayohusika.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msaidizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA
Ataanza mshahara TGS B (1) kwa mujibu wa viwango vya Serikalini.

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II (Nafasi 1)

SIFA/ELIMU/UJUZI

  • Elimu ya kidato cha Nne (IV) , au Kidato cha Sita (VI,)
  • Cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani ya afya, Masjala, Mahakama, na Ardhi.
KAZI NA MAJUKUMU
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
  • Kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu /nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika(classification and boxing)kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki(file racks/cabnet)katika masjala/nyumba za kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kuweka kumbukumbu(barua,nyaraka nk)kataka mafaili.
  • Kushunghulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka taasisi za serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Ataanza mshahara TGS B (1) kwa mujibu wa viwango vya Serikalini.

DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 1)

SIFA/ELIMU/UJUZI
  • Elimu ya kidato cha IV,
  • Mwenye leseni dajara C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka miatatu bila kusababisha ajali.
  • Mwenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja II
KAZI NA MAJUKUMU
  • Kuendesha magari ya abiria na malori
  • Kuhakikisha na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote,na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
  • Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari
  • Kutunza daftari la safari “log-book” kwa 0 safari zote.
NGAZI YA MSHAHARA
Ataanza mshahara TGOS A (1) kwa mujibu wa viwango vya Serikalini.

UMRI
Waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.

MAELEZO YA JUMLA
Maombi yote yawasilishwe yakiwa yameambatanishiwa na CV pamoja na nakala za vyeti vya kuhitimu elimu na mafunzo (vyeti vinavyoonyesha kiwango cha kufaulu na sio 'leaving certificate')

MUHIMU
Muombaji anatakiwa atume vyeti vyake halisi na halali kwani uhakiki utafanyika katika vyuo alivyopitia pamoja na Baraza la Mitihani. Udanganyifu wowote ukibainika hatua za kisheriaz zitachukuliwa

MAOMBI YATUMWE KWA ANWANI IFUATAYO:-

MKURUGENZI WA MANISPAA​
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE​
S.L.P 46343​
DAR ES SALAAM​

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Ijumaa tarehe 22/4/2019 saa 9.30 Alasiri.

Imetolewa na

Lusubilo mwakabibi
MKURUGENZI HALMASHAURI
MANISPAA YA TEMEKE

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)