Nafasi ya Kazi: Mhuduma wa Ofisi na wateja

Habari wanajukwaa, tunahitaji kijana kwa ajili ya kuhudumu kwenye ofisi yetu. Kazi utakazokua unafanya ni kama ifuatavyo:-
  • Kupokea simu za wateja na kuwahudumia.
  • Kutafuta wateja kwa njia ya mitandao ya kijamii na kuwatembelea sehem zao.
  • Kutuza kumbukumbu za ofisi .
Vigezo
  • Awe na elimu ya kidato cha nne au sita. (Mwenye cheti anaweza kupewa nafasi)
  • Ajue kuzungumza kiswahili na kuandika kwa ufasaha.
  • Ajue kutumia mitandao ya kijamii na "Computer"
Kama unakidhi vigezo hivyo, tuma ujumbe mfupi ukielezea wasifu wako kwenda namba 0658123748. Tafadhali usipige simu.
Pia ukituma ujumbe mfupi tujulishe na mahali unapoishi, lengo ni kupata mtu anayeishi maeneo ya jirani na ofisi yetu ilipo kuepusha adha ya usafiri.

Mlo mmoja wa siku utatolewa na ofisi, pia posho ni mpaka Shilingi Laki Moja kwa mwezi. Pia kutakuwa na bonus za kila mwisho wa wiki kulingana na utendaji kazi na kufikia viwango utakavyopangiwa.

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya tarehe 11/04/2019 saa tatu na nusu usiku.
 

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)