Karibu tena mpenzi msomaji wa blog hii, nadhani mpaka sasa umeweza
kupata angalau mwanga wa kujua na kuilinda biashara yako ili iwe yenye
tija na yenye kukua kila siku, leo nitakwenda kuzungumzia hasa aina za
biashara na muundo wake ili kukuwezesha kujua ni aina gani hasa ya
biashara unafanya. Kimsingi kabisa tuna aiana kuu tatu za biashara;
- Biashara za huduma,(Service Business)
Hizi ni aina ya biashara ambazo hujishuguisha na mauzo ya bidhaa
zisizoonekana wala kushikika mf; huduma za elim, afya, ushauri wa
kitaalam, ambapo katika biashara hii pia imegawanyika katika sehem kuu
tatu pia
- Huduma za Kitaalam mf; sharia, ushauri wa maswala ya fedha n.k
- Huduma za Kifedha(Financial Service) mf; bima, benki
- Huduma za Mawasiliano(Information Service
- Biashara ya kuuza bidhaa(Merchandise Business)
Hizi ni aina za biashara ambazo hujishugulisha na kununua bidhaa kwa
jumla na kuuza kwa rejareja, bidhaa hizi ni lazima ziwe zinashikika na
kuonekana kwa macho, aina hii ya biashara ni maarufu kwa jina la
“BIashara za kuuza na kununua”
- Biashara mseto(Hybrid Business)
Hizi ni aina za biashara ambazo zinakuwa zimechangamana kwa pamoja,
biashara hizi huusisha pande mbili ambazo ni utoaji wa huduma na kwa
muda huohuo huuza bidhaa kwahiyo mmiliki wa biashara hii inaweza kutumia
huduma ambazo hazimwingizii faida ila huku akiwa anauza bidhaa ambazo
zitakuwa zinamwingizia faida. Mf; unaweza ukawa unafanya biashara ya
kuuza dawa za binadamu ila kwa wakati huohuo unatoa bure huduma ya
ushauri wa maswala ya afya, kumbuka wapo watu ambao wao wanauza dawa tu
pia wapo ambao wamejikita katika ushauri wa kitaalam juu ya afya, kwa
hiyo utakuwa unapata faida katika kuuza dawa ila ile huduma ya ushauri
unatoa bure.
MIUNDO YA BIASHARA
Kuna mifumo mikuu mine(4) ya kibiashara japo kuna mingine inaibuka ila inaweza kuwa inapatikana ndani ya mifumo hii tajwa;
- Biashara ya mtu mmoja(Sole Trade)
Hii ni biashara ambayo humilikiwa na kuendeshwa na mtu mmoja, yeye
anakuwa kila kitu kwenye biashara hiyo, hasara na faida huja kwake, aina
hii ya biashara humfanya mmiliki hata kuweka rehani mali zake binafsi
ili kulipa madeni(Unlimited Liabilities), kama biashara ikifa au
kufirisika na mmiliki akiwa na deni la nje basi mali zake binafsi
huwekwa rehani ili kulipa deni mf; nyumba, shamba, vitu vya ndani n.k
- Biashara za ushirikiano(Partnership Business)
Hii ni biashara ambayo hujumuisha watu kuanzia 2-19 ambao watu hawa
hupaswa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara(Partnership Deed)
hili ni kalabrasha ambalo huanisha utaratibu wote kuanzia mtaji wa
biashara, mgawanyo na jinsi ya mjumbe kujitoa kwenye muungano husika wa
biashara pia hutoa ufafanuzi juu ya aina ya washirika. Biashara za aina
hii pia hukopeshwa na endapo ikifirisika basi wamiliki hupaswa kuuza
mali zao binafsi binafsi ili kulipa deni(
Unlimited Liabilities Partners) ila wapo pia ambao mali zao hazitaguswa kutokana na ulipaji wa deni hawa wanaitwa (
Limited Liabilities Partners).
- Kampuni(Limited or Unlimited Liabilities Company)
Biashara ya aina hii tunaigawa katika makundi mawili, makampuni
binafsi ambayo kwa mujibu wa sharia ya uwanzishaji wa makampuni hapa
nchini yanapswa kuundwa au kumilikiwa hisa zake na watu kuanzia 7-50 na
watu hawa lazima wawe na mahusiano ya karibu sana, wawe ndugu, jamaa au
marafiki na makampuni ya umma ni yale ambayo hisa zake au amana zake
zinamilikiwa na watu tofauti tofauti kuanzia watu 7 mpaka kuendelea
anayekuwa anamiliki idadi kubwa ya hisa ndie mwenye maamuzi makubwa
Zaidi, ndani ya biashara hizi kuna vitu viwili ambavyo hutoa mwongozo wa
namna yake ambavyo ni
Articles Of Association na
Memorandum Of Association. Kampuni
ambayo huuza hisa kwa umma hutafsiriwa kama kampuni ya umma(Public
Company) ambazo huuza hisa kwa watu wa karibu hutafsiriwa kama kampuni
binafsi(Private Company)
- Biashara za ushirika(Cooperative Business)
Hizi ni biashara ambazo watu huungana kwa pamoja kwaajiri ya kufanya
jambo Fulani na watu hawa huwa wana mtazamo au malengo sawa, mf;
wazalishaji kadhaa ya maligafi fulani wanaweza kuungana pamoja kwa lengo
la kuzalisha maligafi hizo kisha kugawana kulingana na mahitaji yao au
wafanyabiashara wanaweza kuanzisha benki moja kwaajiri ya kuitumia
kurahisisha maswala yao ya kifedha benki hiyo inaweza kuwa na lengo kuu
la kutoa msaada wa kifedha kwa makampuni hayo au pia kusaidia
mabadilishano ya biashara kama wapo ambao wanafanya biashara za
kimataifa kwa hapa Tanzania kuna benki moja ya Ushirika wa Wakulima
inaitwa
Farmers’ Cooperative Bank, Benki hii
ilianzishwa ili kusaidia wakulima kupata urahisi wa mitaji na kuuza
mazao yao katika maduka ya serikali(Sociaty) za vijiji kwahiyo benki
hiyo ilisimamia kila kitu cha kifedha kuhusu wakulima.
Aina zote nilizozitaja hapo juu zinafaida na hasara katika uendeshaji
wake, Mungu akijaalia naweza kuzileta ili uzijue na ujue ni biashara
gani inafaa wewe kuifanya au kuendelea nayo, kufikia hapa nadhani
umepata mwaka kwamba ni aina gani ya biashara unafanya au unataka
kuifanya.
Comments
Post a Comment