Posts

Showing posts from October, 2019

AGIZO KUAPDATE TAARIFA ZA KAMPUNI/JINA LA BIASHARA NDANI YA SIKU 90 NJOO TUKU SAIDIE

TAARIFA KWA UMMA Dar es Salaam, 27 septemba 2019 Hii ni kuutarifu umma kuwa WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (BRELA) inaendelea na zoezi la ihuishaji wa Taarifa za makampuni yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa Kieletroniki. Tunapenda kutoa taarifa kwa umma na watu wote wenye makampuni na Majani ya Biashara kuhakikisha wanauhisha taarifa za makampuni yao na Majina ya Biashara katika kipindi cha SIKU 90 kuanzia tarehe ya tangazo hili. MAHITAJI NA TARATIBU ZA UHUISHAJI WA TAARIFA • Muombaji awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN) ambayo husaidia kufungua akaunti ya BRELA kwenye tovuti ya Wakala. • Endapo maombi ni ya Kampuni unatakiwa kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (Tax Identification Number –TIN) ya kila Mkurugunzi na ya Kampuni husika. • Kupitia taarifa za Kampuni na kuhakikisha zipo sahihi kisheria na kikanuni. • Kujaza ‘Consolidated form’ katika mfumo wa ORS na kupakia taarifa zozote zinazohitajika mfano Taarifa ya Mwaka (Annual returns), mabadilik