Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)

Utangulizi
Kuelekea maendeleo ya sayansi na teknolojia (teke linalokujia) na hasa kwenye nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) makampuni na waajiri wengi sasa wanataka maombi ya kazi yafanywe kwa email au barua pepe (sio barua pepo)
Maombi ya kaz kupitia email husaidia yafuatayo:
  1. kuokoa gharama kama za uchapaji na usafiri
  2. kuokoa muda wa barua kutoka kwa muombaji mpaka imfikie mwajiri
  3. Kuharakisha pia mawasiliano baada ya maombi kutumwa
Kama utaomba kazi kupitia email zingatia yafuatayo:
  1. Tumia email yenye majina yako rasmi. Mfano kama wewe ni Theodory Edmund Ngonyani, email iwe hivi. theodoryngonyani@yahoo.com, theodoryngonyani@outlook.com NK. Angalau majina yako mawili yatokee kwenye email ID. Unaweza hata kuongeza namba kama majina yako mawili hayapatikani. Kumbuka hii itaongeza kuaminiwa na mwajiriwa mtarajiwa kuliko kutumia email kama dumelamji@gmail.com au dijose@gmail.com NK
  2. Tumia pia email zenye kufuata weledi wa kimataifa. Mfano siwashauri watu kutumia email za microsoft, yahoo au zinginezo ambazo zinatumia very offesnive security blocking policy. Mfano halisi ni huu email za Microsoft zinaongoza kwa kublock makun di mengi ya email duniani. Kwa hiyo ikitokea umetumiwa email na mwajiri ambaye email zake zimezuiwa na Server za microsoft ni wazi huo ujumbe wa kuitwa kwenye usaili hautakufikia na hivyo utakuwa umekosa hiyo kazi. Yahoo nao kwa mbali wanafuata. Gmail ndio mtoa wa huduma za email pekee yake ambaye hazuii email yeyote ila anatumia kitu kinachoitwa kwa kimombo “Intelligent Email Blocking Engine” email zako kama zinatia wasiwasi zinapelekwa kwenye spam folder.
  3. Elezea vizuri kwenye kichwa cha habari yaani subject ya email unaomba nafasi ipi ya kazi. Wengine wanatoa kabisa kichwa cha somo kwa hiyo unatakiwa kukopi na kupaste. Usipofanya hivyo maombi yako yanaweza kuachwa na system kwani email kama hizi zinachujwa na mfumo wa kielectroniki kwa hiyo ukikosea kidogo tu imekula kwako wewe mwombaji.
  4. Kwenye email body au mesage eleza wewe ni nani? Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi?Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi) Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi. Pia eleze kjwa ufupi:Kiwango chako cha elimu (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba) Uzoefu wako wa kazi (elezea tu ya hivi karibuni na inayoendana na kazi uliyoomba)Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani). Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wakotu (usiambatanishe vyeti au kitu kingine kwani hivyo utavipeleka wakati ukiitwa kwenye usaili)
  5. Weka viambatanisho tu ambazo ulielekezwa utume, vile ambavyo hukuambiwa usitume maana vinaweza kukukosesha kazi. Waajiri wengi siku hizi wanapunguza mzigo wa maombi ya kazi ikiwa ni pamoja na package nzima ya maombi lakini pia na wingi wa waombaji. Ni rahisi sana kuchujwa kwenye chujio la mwanzo kama wewe umekiuka masharti ya wazi tu. Nasema ni rahisi kwa sababu waombaji ni wengi kwa hiyo waajiri wana aina fulani ya kuringa.
  6. Kwenye viambatanisho hakikisha vyote vina majina yanayoendana na kilichomo ndani. Mfano kama umeambatanisha Barua ya Maombi ya Kazi ya Mhasibu Msaidizi, weka jina la faili liwe na hayo maneno. Kama umeambatanisha CV kwenye filename ya CV weka CV ya …jiana lako NK

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email

Yah:  Maombi ya Kazi ya ………………………………………………………………..(hii inawekwa kwenye email subject)
Simu:0764530882
Emal: bizewiseconsultancy@gmail.com
31/1/2019
Ndg………………………………………….
Husuika na kichwa cha somo tajwa hapo juu, mimi ni mhitimu wa sheria kutoka chuo cha ……………………… nimefanya kazi kwa miaka miwili na nina usoefu kwenye sheria za makampuni na ajira. Napenda sana kujifunza mambo mapya na nina hamu ya kuleta mabadiliko kila mara. Tabia hii nimejijengea tangu utotoni kwani wazazi wangu walikuwa wakiniita mtoto mdadisi kwa sababu ya tabia hii ya kupenda kujau na kufanya jambo jipya kila mara.
Nimeambatanisha barua ya maombiu ya kazi na wasifu wangu katika barua pepe hii
Kwa mawasiliano ya hara tafadhali piga namba hii (7564530882) wakati wote isipokuwa usiku wa saa nne mpaka 12.00 asubuhi
Nitafurahi nikiitwa kwenye usaili ili nidhihirishe kwako jinsi nitakavyowafaa kwenye kampuni yeni pendwa
Wako
Jina Langu
Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Kupitia Email kwa Kiswahili

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI