EWE MJASIRIAMALI, HATUA ZA KUUNDA KAMPUNI HIZI HAPA, MILIKI KAMPUNI SASA.
Na MTAALAMU WAKO STEP 1; chagua jina. Kampuni lazima iwe na jina linalotambulika na linalojitofautisha na majina ya makampuni mengine nchini. Hatua hii, kwa lugha ya biashara huitwa ‘Name Search’ ambapo unatakiwa kutumia online account ya Brela kuuliza iwapo jina ulilochagua linafaa na hakuna linapotumika Tanzania. Jina hilo litaingizwa kwenye mtandao wa makampuni yaliyosajiliwa na Brela, ili kuona kama kuna kampuni yenye jina linalofanana na hilo lako. Kwa kuwa majina yote ya kampuni nchini yako ofisi hiyo, hivyo si rahisi kampuni zaidi ya moja kuwa na majina yanayofanana. Ikibainika kuwepo kwa kampuni yenye jina kama la kwako, Ofisa wa Brela, atakuelekeza utafute jina jingine, na kama atakuta hakuna jina la kampuni linalofanana na la kwako, basi jina hilo litapokelewa kwa hatua inayofuata. STEP 2; andaa waraka na katiba ya kampuni (memorundum&article of association). Baada ya jina kuwa limethibitishwa, kwa maana ya kukubaliwa na Msajili wa Kampuni, hatua in...