TAARIFA KWA UMMA KUFUTWA KWA MAKAMPUNI (LIMITED BY GUARANTEE) YENYE KUFANYA SHUGHULI ZILIZOAINISHWA KWENYE SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGO’S)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (Ofisi: Jengo la Ushirika Mtaa wa Lumumba) Simu: +255-22-2181344, 2180113, 2180141 2180048, Nukushi:+255-22-2180371 Barua Pepe: usajili@brela.co.tz ceo@brela.go.tz brela@brela.go.tz S.L.P. 9393 DAR ES SALAAM. TAARIFA KWA UMMA KUFUTWA KWA MAKAMPUNI (LIMITED BY GUARANTEE) YENYE KUFANYA SHUGHULI ZILIZOAINISHWA KWENYE SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGO’S) 1. Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Makampuni (SURA.212 ) yaliyofanyika kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na. 3) ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa tarehe 30 Juni 2019, Jukumu la kusajili Makampuni yanayofanya shughuli kwa lengo la kutogawana faida na ambazo hazina malengo ya kukuza biashara” promotion of commerce” limehamishiwa kutoka kwa MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA) kwenda Kwa Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s). 2. Kufuatia mabadiliko haya, MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA) anapen...