HATUA 10 ZA USAJILI KUTOKA BRELA-0764 530 882



Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BREAL. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu wa
mawasiliano

HATUA 10 ZA USAJILI
Hatua #1: Taarifa za msajili
  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni (Company Information)
  1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
  2. Jina la kampuni
  3. Kazi zitakazokuwa zikifanywa na hiyo kampuni tarajiwa (Activity description)
Hatua #3: Ofisi za kampuni (Office Location)
  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa.
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, namba ya kitalu na namba ya nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe (email)
Hatua #4: Shughuli za Kampuni (Company Activities)
Hatua #5: Taarifa za Wakurugenzi (Directors Information)
  1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni (Company Secretary)
  1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa (Subscribers Information)
  1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
  1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
  4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
  1. Kusajili kampuni
  2. Kuhifadhi nyaraka na
  3. Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni
  1. Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money na HaloPesa
  2. Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo.

HITIMISHO NA USHAURI

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:
  1. Nashauri kama unataka kufanya usajili wa Haraka na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia.
  2. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho.
  3. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kusajiliwa kampuni au jina la biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia kwenye ukurasa huu au 0764 530 882/0717 756 853

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)