INAHUSU KILIMO BORA

MATUMIZ YA MBOLEA ZA KUKUZIA KWENYE MAHINDI
        Mbolea za kukuzia ni mbolea zinzotumika kuupa mmea afya nzur na mavuno kuwa mazuri wakati wa kuvuna. mbolea hizi zikitumika vibaya pia huleta madhara makubwa kwa mlaji na ardhi kwa ujumla, zipo mbolea za aina nying lakin leo nitazungumzia
   CAN na
   UREA.
hizi ni mbolea ambazo zinapatikana kwa urahisi na wakulima weng hupenda kuzitumia katika kukuzia mimea yao kama mahindi maharage viazi na n.k
   
       JINSI YA KUTUMIA KWA VIPIMO
 tumia mfuko mmoja waa kg 50 kwa ekari moja uishe wote, weka kwa vipimo maalumu na kwa usahihi ili kupata mavuno bora
    weka  mbolea mara mbili kulingana na ahali ya mazao yako, anza na mbolea ya UREA ili kuupa mmea afya nzurio a kukua araka, baada ya hapoo  tumia CAN pale mahindi yanapokaribia kueka mtoto au gunz ili kuupa uwezo wa kueka punje kubwa na imara kwa gunz lote bila kubakisha.
   weka g5-10 kwa kila mmea nfdani ya shamba lakoo ili kusaidia kupata mavuno mengi
 UREA hubeba nitreogen kwa wingi
 CAN husaidia kuongeza calcium kwenye mmea
    mbolea zipo za aina nyingi zingoine pia ni nzur lakini zitumike kwa vipimo maalumu ili kuto kukupa hasara kwenye mavuno
    kama utakua unahitaji notsi kwa ajili ya mazao ya kilimo usisite kusema matumizi ya madawa na mbolea

KILIMO CHA PILIPILI HOHO (SWEET PEPPER)
 

    pilipili hoho ni zao ambalo hulimwa sehemu nyingi nchin tanzania na hutumiwa na watu wengi kama kiungio cha mboga na pia hutumika kama mboga chenyewe. hili ni zao ambalo huchukua mda mfupi kukua hadi kuanza kuvunna.  na huvunwa zaidi ya mara tano hadi sita likihudumiwa vizurii.
   
        KUANDAA SHAMBA
 andaa shamba vizuri kwa kulitifulia vizuri na kulimwagia samadi mapema kabla ya kupanda zao hili. unaweza kulima kwa trekta kama unauwezo na jembe la mkono pia laweza tumika ili kufanya maandalizi mazuri ya shamba
    KUANDAA MBEGU
   Andaa mbegu mapema kwenye kitalu safi  ili kuweza kuhamishia kwenye eneo lako badae unapoanza kupanda. si vizuri kuandaa kitalu mbali na eneo ambalo unategemea kupanda mbegu zako. mbegu iachwe ikue vizuri ndipo ihamishwe shambani kwa ajili ya uzalishaji.
    a
AINA ZA MBEGU
    Zipo aina  nyingi za mbegu ya pilipili hoho ambazo hulimwa na hupendwa sana na watu wengi. kwa mfano kuna( psserela) na (illanga) ambazo zinakua na rangi tofauti
     MBOLEA
 Tumia dap kwa kupandia na baada ya hapoo utaeka CAN au UREA kwa kuzia na wakati wa kuanza kutoa maua tumia MOP kwa kuimarisha maua yasidondoke ovyoo. tupia dawa za madudu unapoona wadudu anashambulia mmea wakoo na dawa za ukungu kipindi mimea inapoanza kuathirikaa

    kKUVUNNA
  pilipili hoho huchukua miezi mitatu hadi kuanza kuvuna na kumaliza kuvuna pia hivyo ni zao la muda mfupi na linafaida kubwaa
  hakikisha unaandaa sehem ya kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi kujua kua kilimo kina faida kwako au hasara.

KILIMO CHA MAHARAGE

   ndugu wasomaji napenda kuwaletea aina nyingine ya mbegu ya maharage ambayo ni bora na nzuri kwa kupandwa kwa maeneo yote yanayokubali zao hili. Mbegu hii ilifanyiwa uchunguzi kwenye chuo cha uchunguzi wa mbegu UYOLE Mbeya na kuruhusiwa kwa ajili ya kilimo ndani ya jamii
  Aina ya mbegu tutakayojifunza leo ni

BILFA 16
   Mbegu hii ya maharage ni nyekundu yenye vichirizi vichiriz vyeupe kwa mbali hukua kwenye uwanda uliombali na bahari usawa wa800-2000 kutoka baharini. mbegu hii hukua haraka na huzaa maharage yenye rangi nyekundu na huwa na matawi kuanzia 4-6. Mbegu hii hutoa maua ya pink vishuba au vikoba vyeupena vikikomaa huwa na rangi ya maziwa

KIASI CHA MBEGU NA UZALISHAJI
    Mbegu hii nyekundu hupandwa kilo 70-80 kwa hekta moja ambayo ni sawa na ekari mbili na nusu.mbegu hii huzaa vizuri pia ila inamapungufu ukilinganisha na uyole 04 ambayo ni sawa na miche 205000. kwa hekari moja unapata tani 1.4-1.6 za maharage yaliyoko tayari kama utayalima kitaalam
    Ni vyema kufanya palilizi mapema ili kuyapa maharage sapoti nzuri katika ukuaji wake. ili kupata mavuno mazuri pia ni vyema tuka hudumia vizur zao hili kwa kupuliza dawa pale wadudu wanapoanza kushambulia mimea.

  MDA  WA KUPAND NA KUVUNA
         Mbegu hii ya maharage hupandwa mwezi wa  3 kama mvua zikiwahi na endapo mvua zitachelewa hupandwa mwezi wa nne. Maharage haya huchukua siku 110 kukomaa hadi kuvunwa. Wakati maharage yanapokauaka tu ni vyema kuvunwa ili kukwepa hasara ya kupasukapasuka ovyoo shambani.

     kwa mawasiliano zaidi kuhusu kilimo na ufugaji piga 
sim no 0764530882
email theo350789@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)