Jinsi ya Kuingiza Taarifa za Kampuni Kwenye Website ya BRELA

UTANGULIZI

Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.
Hatua zifuatazo zinawawezesha wamiliki, wasimamizi wa makampuni na biashara kuingiza taarifa zao kwenye tovuti ya BRELA
Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za kampuni chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu 

Hatua #1: Taarifa za msajili

Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la  kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).
Taarifa zenyewe ni:-
  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email

Hatua #2:  Taarifa za kampuni

Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
  2. Jina la kampuni
  3. Kazi zitakazokuwa zikifanywa na hiyo kampuni tarajiwa (Activity description)

Hatua #3:  Ofisi za kampuni

Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-
  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email

Hatua #4:  Shughuli za Kampuni

  • Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification

Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi

Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-
  1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email

Hatua #6:  Taarifa za katibu wa kampuni

Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe – email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email

Hatua #7:  Taarifa za wanachama/wenye hisa

Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-
  1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe – email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo:  Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email

Hatua #8:  Viambatanisho

Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-
  1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
  4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni

Hatua #9:  Ada za usajili na kufaili

Malipo ya ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini
  1. Kusajili kampuni
  2. Kuhifadhi nyaraka na
  3. Stamp Duty

Hatua #10:  Namna ya kulipa ada

Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu mbili ambazo ni
  1. Simu ya mkononi kwa kutumia akaunti za MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa
  2. Kulipa moja kwa moja benki kwenye akaunti zilizopo CRDB au NMB
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo

HITIMISHO NA USHAURI

Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi magumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia.

Nashauri yafuatayo:

  1. Nashauri kama unataka kuingiziwa taarifa za kampuni kwa haraka wasiliana nasi kwa0764530882
  2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.
Kwa wale wanaohitaji kuingiziwa taarifa za kampuni au biashara chapu chapu tafadhali wasiliana nami kupitia namba za simu hapo chini au kwenye ukurasa huu

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)