Kazakh: Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena, baada ya kufukuliwa miaka 50 iliyopita

Tangu uhuru mwaka 1991 amekuwa ni ishara ya urithi wa asili wa taifa huko Kazakhstan. Silaha yake ya dhahabu imekuwa ni kitu cha kujivunia na imehifadhiwa katika hifadhi ya taifa ya Astana, pia hudhuru sehemu mbali mbali duniani kama alama ya tamaduni ya Kazakh.
- Serikali yazima jaribio la mapinduzi Gabon
- Kinywaji kinachodaiwa kuwa na 'Viagra' kuchunguzwa Uganda
'Pumzika kwa amani'
Mifupa ilipatikana tena hivi karibuni katika taasisi ya upelelezi wa mambo ya kale, yakiwa yamehifadhiwa katika boksi huku yakiambatanishwa na karatasi iliyo andikwa "The Golden Man, May He Rest in Peace", yaani "Binadamu wa dhahabu, apumzike kwa amani."
"Tunajua umri wake na maisha yake ya kijamii, wakati kipimo cha vinasaba kinaweza tupatia taarifa nyingi kupita kiasi," mtafiti Dosym Zikiriya anaiambia Kazakh TV.
Lakini Yermek Zhasybayev wa hifadhi ya Issyk ametoa matumaini kidogo sana juu ya upatikanaji wa taarifa. "Mifupa ipo katika hali mbaya. Imehifadhiwa katika box kwa miaka 50 sasa na imekuwa ikikumbana na kila aina ya kakteria na virusi vikiwemo virusi vya sasa. Kwa sasa ni ngumu kupata taarifa sahihi za vina saba - ila kama tungalikuwa na fuvu au walau jino moja," amekiambia kituo kimoja cha televisheni.
"Katika kutambua heshima ya binadamu huyo wa dhahabu, kuzikwa tena kwa mabaki ya shujaa huyo kutaambatana na sherehe za kimila ili kuendana na tamaduni za kifalme za miaka ya nyuma", Kazakh TV imefafanua.
Wanahistoria wanaimani kwamba mabaki hayo ni ya karne ya pili mpaka ya tatu kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, wakati ambao kusini mashariki mwa Kazakhstan ilikuwa ni makazi ya watu wa kabila la Saka, ambao walikuwa wanaaminika kuwa sehemu ya wa Scythian watu wa jamii ya kuhama hama.
- Mungo Man: Mabaki ya kale zaidi ya binadamu yapelekwa nyumbani Australia
- Mji wa kale wa ‘majitu’ wagunduliwa Ethiopia
Anaonekana katika maeneo mengi kama alama ya uhuru kote nchini, ikiwa ni pamoja na mji wa Astana na mji maarufu wa biashara wa Almaty ikiwemo pia kwenye maeneo ya Raisi na sarafu ya nchi hiyo.
'Mwanamke wa dhahabu?'
Taarifa za binadamu wa dhahabu zimegusa jicho la watayarishaji vipindi vya BBC ambao walitengeneza makala ya mwaka 2017 iliyotangazwa na mwanahistoria Bettany Hughes.
Lakini inaaminika kuwa vipimo vya vinasaba vya kizazi kijacho huenda vikatatua maswali kama je ni mwanaume wa dhahabu au mwanamke wa dhahabu?
Watafiti wa mambo ya kale wanasema mpaka sasa hakuna uthibitisho kutokana na asili ya utafiti wa mabaki kwani kuna mabaki yaliwahi kupatikana katika mfumo huo ambayo yalikuwa ni ya kaburi la mwanamke kusini mwa Urusi.

Comments
Post a Comment