Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq
Rais wa Marekani
Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya
krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.
Walisafiri
kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa
huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa White house.Bw Trump alisema Marekani haina mpango wa kuondoka nchini Iraq.
Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo.
Hata hivyo mkutano uliopangwa kati ya Bw Trump na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ulifutwa. Ofisi ya Bw Mahdi ilisema hiyo ni kwa sababu ya kutokubaliana jinsi mkutano huo ungefanyika.
Mazungumzo kwa njia ya simu kati ya viongozi hao badala yake yalifanyika na White House inasema Bw Mahdi alikubali mwaliko kwa kuzuru Marekani.
Kipi kilifanyika wakati wa ziara ya Trump?
Ndiyo ziara yake ya kwanza ya aina hiyo eneo hilo.
Wakati wa ziara hiyo alipata makaribisho mazuri kutoka kwa wanajeshi wakati aliingia ukumbi wa maankuli na kutembea akiwasalimia wanajeshi na akipigwa picha nao.
Alisema sababu ya ziara hiyo ni kuwashukuru mwenyewe wanajeshi kwa kusaidia kuwashinda Islamic State.
Comments
Post a Comment