Mtaalamu bingwa wa afya ya akili kutoka Tanzania kutuzwa Marekani
Mtaalamu bingwa wa afya ya akili kutoka Tanzania kutuzwa Marekani
Mtaalam bingwa wa
kukabiliana na matatizo ya kiakili na mtafiti kutoka Tanzania Profesa
Sylvia Kaaya ni miongoni mwa watu sita ambao watatuzwa shahada ya
heshima na chuo cha Marekani cha Dartmouth.
Profesa Kaaya kutoka
chuo cha Afya na Sayansi cha Muhimbili {Muhas}, ni miongoni mwa wataalam
60 wa kukabiliana na matatizo ya kiakili nchini Tanzania anayeangazia
kuendeleza vitendo vinavyoweza kufaidi mataifa yalio na raslimali
chache, kulingana na duru za gazeti la The Citizen nchini Tanzania.- G7: Trump atofautiana na washirika wake
- Mtanzania anayetarajiwa kufanikiwa katika teknolojia
- Kwa nini Malkia Elizabeth 'ana siku mbili za kuzaliwa'
Kila anayetuzwa atapewa shahada ya heshima ya Udaktari .
Taaluma za wataalam hao zinaangazia maswala tofauti kutoka burudani, huduma kwa jamii hadi matibabu.
Miongoni mwa wale watakaotuzwa ni pamoja na wadhamini wa taasisi hiyo pamoja na mshirika wa Goldman Sachs aliyestaafu Peter fahey , mbunge wa zamani na mwakilishi katika Umoja wa mataifa Frank Guarini ambaye ni afisa wa matibabu pamoja na daktari a upasuaji Williams Holmes, Muigizaji , mtayarishaji na mwandishi Mindy Kaling na Mwanzilishi pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Carlyle David Rubenstein.
Comments
Post a Comment