Namna Ya Kukuza Na Kuendeleza kipaji Chako

Kipaji au talanta kwa maana nyingine ni uwezo ambao binadamu anapewa na Mungu wa kufanya mambo mbalimbali hapa duniani.Vipaji hivi vinatofautiana baina ya mtu na mtu japokuwa kwa baadhi ya watu vinafanana.Kuna watu wana vipaji vya kuimba,kuchekesha,kuchora,kuigiza ni vingine vingi ambavyo havijatajwa hapa.
Kwa ujumla kila mtu hapa duniani amepewa kipaji fulani,wapo walioweza vipaji vyao mapema,wapo waliochelewa kugundua na wengine wameshindwa kabisa labda kutokana na mazingira wanayoishi au sababu kadha wa kadha.Leo hii nitakushirikisha namna ya kugundua na kukiendeleza kipaji chako ambacho mda mrefu umekuwa ukijiuliza kipaji chako ni kipi.


Namna ya kuendeleza kipaji chako
1.Lazima ujue vipaji vyako
Unatakiwa ujitathimini nguvu na uwezo wako .Familia na marafiki zetu wanaweza kukusaidia kufanya kazi hii kwani ndio unaishi nao muda mwingi.Andika vitu unavyoweza au unavyotaka kufanya.Hii itasaidia kujua vitu tunapenda na tunafanya vizuri zaidi.Unatakiwa pia kumwomba mwenyezi Mungu akusaidia kuhusu vipaji vyako.


2.Lazima ukubali kuwa tayari kutumia muda na uwezo/nguvu zako zote kukuza vipaji.
Usikate tama kama hufanyi vizuri katika ikuzaji wa kipaji chako.Watu wengi wanaishia njiani katika swala zima la kukuza vipaji kwa sababu wanataka tamaa mapema pindi wanapofanya vibaya au kuchekwa na watu. Nina mfano mzuri wa Kevin Hart ambaye alipoanza sanaa ya kuchekesha watu walikuwa wanampiga na pizza na kumcheka kuwa hawezi aache tu,hakukata tamaa aliendelea na sasa ni mchekeshaji maarufu duniani.


SOMA:Umuhimu wa kuwa na marafiki


3.Lazima uamini kuwa unaweza
Wewe kama wewe lazima ujikubali na uone kuwa kipaji chako watu wengi wanakihitaji marafiki zako,familia yako na ulimwengu kwa ujumla.Usioogope kukionyesha,pambana mpaka mwisho kama tunahitaji msaada tuulize kwa watu wenye vipaji kama hivyo.Hapa nitakupa mfano wa Stevie Wonder ambaye ni mlemavu wa macho lakini kwa kuamini kuwa anaweza pamoja na ulemavu wake alipigana mpaka kuwa mwanamuziki maarufu ambaye dunia inamtambua.Wewe ambaye umejaliwa kila kitu huna tatizo lolote kazi kwako.


4.Lazima ujifunze ujuzi ili kuendeleza vipaji vyako.
Utafanya hivi kwa kwenda shule,kufundishwa na rafiki au kusoma kwenye vitabu. Usiogope kujichanganya na watu mbalimbali ambao wanaweza kuona kipaji chako na kukushauri mambo baadhi na wewe kujifunza mengi kutoka kwao.Kwa mfano mimi namfahamu mtoto mmoja ana kipaji cha kuchora michoro mbalimbali kwa ustadi kabisa lakini hajui kuipaka rangi ili ipendeze,na mwenyewe anakiri kuipakaka rangi mbalimbali hawezi.Mtoto kama huyu anahitaji elimu kidogo aidha ya darasani au kufundishwa na rafiki yake au yeye mwanyewe kusoma kwenye vitabu.


5.Lazima ufanyie kazi vipaji vyako.
Kila kipaji kinahitaji nguvu na kufanya kazi kwa juhudi.Ili kipaji chako kiweze kufanikiwa vizuri lazima ukifanye kila siku ijao kwa Mungu.Kwa kufanya hivi itakufanya ukipende na kuwa na moyo nacho.Watu wengi sana ni mimi nikiwa miongoni tumeuwa vipaji vyetu vingi kwa kuwa wavivu wa kufanyia kazi vile vitu tulivyokuwa tunavifanya tukiwa watoto.Mimi nakumbuka wakati nikiwa mdogo kwenye michezo ya utoto nilikuwa naweza kufanya mambo mengi kiasi kwamba ningeweza kuendelea kuvifanya mpaka ukubwani dunia ingekuwa inanitambua.


6.Lazima ushirikishe watu wengine vipaji vyako.
Kwa kutumia vipaji vyako ndo vitakua.Kama kipaji chako kiko tayri usikifiche,waonyeshe watu wakione kuwa una kipaji fulani.Kwa kufanya hivi ulimwengu mzima utakutambua na utapata mafanikio zaidi.Ukiwa na tabia ya uchoyo kwa kweli kipaji chako hakitaonekana badala yake kitakufa kabisa.


N.B.Kama una kipaji fulani bado muda wa kukionyesha unaruhusu haijalishi umri wako.
 

Comments

Popular posts from this blog

Barua ya Kuomba Kazi

ANDIKO LA MRADI WA KUOMBA UFADHILI

Barua ya Maombi ya Kazi Kupitia Email (Barua Pepe)